Description
1977 - 1983
Sweden, Stockholm
Ambassador
Balozi Mhina aliwahi kuwa Mkuu wa shule ya kati/sekondari wa Kwanza Mwafrika huko Malangali - Iringa,Aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Elimu Kibaha kabla ya kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu.
Mwaka 1972/73 Mwalimu Nyerere, alimteua kuwa Balozi wetu huko Scandinavia (Sweden, Norway, Finland na Denmark), alikaa Sweden kwa kipindi cha Miaka 10 na kurudi Tanzania 1984. Alipokuwa Stokholm alikuza kwa kiwango kikubwa Ushirikiano wetu na Sweden...Familia yake ina urafiki wa karibu na Familia ya Marehemu Waziri Mkuu olof Palme.
Aliporudi Tanzania alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Elimu na Baadaye kuwa Mwenyekiti kwenye Bodi ya SIDO.