Description
Japan, Tokyo
Ambassador
Mathias Meinrad Chikawe (born 30 May 1951) is a Tanzanian CCM politician and Member of Parliament for Nachingwea constituency since 2005.
- Ambassdor of the United Republic of Tanzania in Tokyo, Japan who is also accredited to Australia, New Zealand and Papua New Guinea 2016 - 2019
- 21st Minister of Home Affairs 20 January 2014 – 5 November 2015
- Minister of Justice and Constitutional Affairs 7 May 2012 – 20 January 2014
- Minister of State in the President's Office for Good Governance 28 November 2010 – 7 May 2012
Alma mater
- University of Dar es Salaam
- North Staffordshire Polytech.
- ISS (PGDip)
HISTORIA
Mathias Meinrad Chikawe anasema alizaliwa mwaka 1951. Alipata elimu ya awali (chekechea) katika Shule ya St. Josephs Convent ya jijini Dar es Salaam mwaka 1958.
Alipata elimu ya msingi shuleni hapo kati ya mwaka 1959 na 1965 kabla ya kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule hiyo hiyo mwaka 1966 hadi mwaka 1969 alipohitimu kidato cha nne.
Kati ya mwaka 1970 na 1971 alipata elimu ya sekondari ya juu (kidato cha tano na cha sita) katika Shule ya Mkwawa iliyopo mkoani Iringa. Mwaka 1972 alijiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Ruvu, kabla ya kuchaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi mwaka 1975 alipohitimu digrii ya sheria.
“Mwaka huo huo wa 1975 mara baada ya kuhitimu chuo kikuu niliajiriwa katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, huku nikipata mafunzo ya vitendo pia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Shirika la Sheria Tanzania na Chuo cha Siasa Kivukoni hadi mwaka 1976 nilipohitimu nikaajiriwa rasmi na kupangiwa kazi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,” anasema Chikawe.
Baadaye alihamishwa kwenda kuwa Mwanasheria wa Wizara ya Kilimo, akiwasaidia John Malecela na Joseph Mungai katika kipindi cha miaka 10 kabla ya kuhamishiwa Ikulu ambako alifanya kazi kati ya mwaka 1985 na 1998, kabla ya kuanza kujitosa kwenye siasa mwaka 1999.