Description
Congo (DR), Kinshasa
Ambassador
USSR, Moscow
Ambassador
Paul James Casmir Ndobho alizaliwa mwaka 1938, Efulifu, Musoma mkoani Mara, hivyo hadi mauti yanamkuta alikuwa na miaka 81. Alipata elimu yake seminari iliyoko Nyegezi, Mwanza na kisha kujikita kwenye vyama vya ushirika kabla ya kuingia kwenye ulingo wa siasa.
Ubunge
Oktoba mwaka 1965, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa inafanya Uchaguzi Mkuu katika mfumo wa chama kimoja cha Tanganyika African National Union (TANU), Ndobho akiwa mwanachama wa TANU, alijitosa katika kinyang’anyiro cha ubunge Jimbo la Musoma Kaskazini. Akiwa kijana mdogo tu wa miaka 27 mwaka huo, alikonga nyoyo za wapiga kura na kuibuka mshindi, hivyo kutangazwa kuwa Mbunge wa Musoma Kaskazini.
Ateuliwa Katibu wa TANU Kigoma
Februari, 1970, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Nyerere, alimteua Ndobho, aliyekuwa na michango iliyosheheni ‘madini’ bungeni, kuwa Katibu wa TANU Mkoa wa Kigoma. Wadhifa huo, kwa utaratibu wa enzi hizo, ulimfanya pia kuwa mkuu wa mkoa na mbunge.
Ndobho aliwatumikia wananchi wa Mkoa wa Kigoma hadi Novemba, 1975.
Ateuliwa Balozi Urusi
Machi 2, 1976, Rais Nyerere alimteua Ndobho kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi kwenda kuchukua nafasi ya Balozi Cecil Kalaghe aliyerudishwa nyumbani. Hivyo, mara moja Balozi Ndobho akaondoka nchini na kwenda kuanza kuhudumu kama mwanadiplomasia huko Urusi.