Description
Mozambique, Maputo
High Commissioner
H.E. Shamim Nyanduga High Commissioner of the United Republic of Tanzania in Maputo, Mozambique, who is also accredited to The Kingdom of Eswatini and Madagascar. December 18, 2011 - 2017
Balozi Nyanduga alikwenda nchini Australia mwaka 1994 kwa ajili ya mafunzo ya Shahada ya Pili na alihitimu mwaka 1995 na alirudi kuendelea na kazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, mpaka mwaka 2000 ambapo alikwenda kikazi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini mpaka 2005, ambapo alirudi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kufanya kazi Idara ya Afrika.
Akiwa bado wizarani, Balozi Nyanduga ndio alikuwa Mratibu wa Mkutano wa kimataifa wa Sullivan na aliendelea kupanda cheo na kuwa Naibu Mkuu wa Itifaki, cheo ambacho alikuwa nacho hadi alipoteuliwa na Rais mwaka 2011 kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji. Balozi Nyanduga ambaye anazungumza vizuri lugha ya Kireno, lugha inayotumika zaidi kwa mawasiliano Msumbiji, ni mke wa Bahame Tom Nyanduga, ambaye mapema mwaka huu Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Wamejaliwa watoto wanne.